Social Icons

Thursday, December 22, 2011

UHURU WA KUABUDU

UHURU WA IBADA/ IMANI/ DINI NA KUABUDU KWA VIJANA WA TAASISI ZA ELIMU NA RAIA KAMA ULIVYOBAINISHWA KATIKA KATIBA MAMA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ambassador’s Congress 25th Dec 2010- Y.I. Juma

KUSUDI LA SOMO:


  1. Kusaidia vijana wetu wa kanisa kujenga uimara wa imani yao kwa Mungu, Ujasiri wa mahusiano yao na Mungu katika hali zote za maisha, kazini, Biashara, Taasisi za elimu na mtandao mzima wa shughuli za maisha zinazoweza kuathiri mahusiano yao ya ki-imani na kuwalazimisha kufanya kazi/ Kusoma/ kufanya biashara au burudani na michezo isiyo na maadili siku ya sabato au kinyume cha imani yao kwa ujuzi wa kuielewa sheria ya nchi na sauti ya Mungu Math 22:21-22, Warumi 13:1-8, 1Petro 2:13-17
  2. Kuwasaidia vijana wa kanisa kusimama imara katika imani kwa zamu yao bila tegemezi la mtu yoyote, awe mchungaji , mzazi au kanisa. Imani aliyoielewa aisimamie kwa dhati hata katikati ya moto. Daniel 3:16-18

UJUZI WA KISHERIA NA WA-KIIMANI KATIKA KULINDA IMANI YA VIJANA WA KANISA

1. Ni heri kumtii Mungu kuliko Mwanadamu- Matendo 5: 29

2. Jua haki ya Kikatiba na Sheria ya nchi ya kila raia katika swala zima la kuabudu na kushiriki shughuli za Ki-imani.

3. Jua wajibu wako katika kujihusisha na mambo ya imani na ibada

4. Jua nini cha kufanya haki yako ya ibada/imani inapokiukwa makusudi na mamlaka iliyo chini yako.

5. Jua hatua za kisheria na za-kinidhamu zitakazochukuliwa dhidi yako kwa kukiuka wajibu wako katika maswala ya imani.

DONDOO NA NUKUU ZA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA MASWALA YA IMANI NA IBADA

  1. Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchunguzi katika mambo ya dini’ Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6[1]
  2. Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za Mamlaka ya nchi. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6
  3. Kila palipotajwa neno “ dini” katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6
  4. Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayohusu Taifa. Uhuru wa Kushiriki shughuli za umma: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6

VIJANA WA KANISA NA TAASISI ZA ELIMU NA WAJIBU WAO KATIKA KUTII SHERIA ZA NCHI

Wajibu huu ni kwa mujibu wa katiba kipengele cha “ Wajibu wa kutii Sheria za nchi:

Sheria ya 1984 Na. 15, ib. 6

  1. Ni wajibu wa kisheria na agizo la Mungu vijana kufanya kazi halali za mapato au za jamii bila kuvunja sheria ya nchi na Sheria ya Mungu.
  2. Ni wajibu wa Kisheria na agizo la Mungu kutii sheria halali za nchi bila kumkosea Mungu.
  3. Ni wajibu wa Kisheria kulinda mali za umma na kuepuka hali zote za machafuko na kualifu amani ya jamii kwa nia ya kuhujumu mali za umma unazozitumia.
  4. Ni wajibu wa Kisheria kulinda na kusimamia ulinzi na usalama wa raia katika mambo yote, likiwapo swala la ibada.

BIBLIA NA MIFANO YA WATU WALIOSIMAMIA IMARA IMANI ZAO BILA KUVUNJA SHeRIA YA NCHI WALA SHERIA YA MUNGU

  1. YUSUFU- Mzo 39:9-11 “ Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe” Sheria ya Misri ya Mahusiano ya ndoa na sheria ya Mungu Kutoka 20:14 ‘Nifanyeje ubaya nimkose Mungu’

  1. ESTER- Esta 4:16 “ Nitaingia kwa mfalme, Kinyume cha Sheria; nami nikiangamia, na niangamie” Sheria ya Wa-Amedi na Waajemi isiyobadilika

  1. Daniel- Dan 6:4-5, 8, 10, 16 : Sasa ee mfalme piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Waamedi na Waajemi. Daniel akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

  1. Shadraka, meshaki abednego- Dan 3:16, Dan 3:18 “ Bali kama si hivyo, ujue Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.

  1. Paul: Matendo 22:25- Je ni halali ninyi kumpiga mtu aliye mrumi naye hajahukumiwa bado? Sheria za Rumi

  1. Yesu: Mathayo 10:17-20 “ Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga. Nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa, Msifikiri-fikiri jinsi ya kusema, mtapewa saa ile ile mtakavyosema kwa kuwa Roho atawaongoza kunena

--------------------------------------------------------------

Ambassador’s Congress 25th December 2010, Nyanza Secondary- Pr Juma



[1] Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, Toleo la Julai, 1985

No comments:

Post a Comment