IDARA YA ELIMU-TUCASA UDOM
TAARIFA
YA UTENDAJI KAZI MWAKA 2O12/2013.
Taarifa hii ya
utendaji kazi wa idara ya elimu TUCASA UDOM kwa mwaka wa uongozi 2012/2013
imegawanyika katika sehemu kuu nane( 8) ambazo ni.
1.Utangulizi.
2.kazi na malengo
ya idara.
3.Malengo yaliyofanikiwa.
5. Fedha, bajeti na
matumizi.
6.Changamoto.
7.Maoni na mapendekezo.
8.Hitimisho.
1.UTANGULIZI:
Kwanza kabisa
tunapenda kumshukuru MUNGU kwa uweza
wake wa kutulinda tangu tumeanza uongozi
mpaka leo tunapofikia hitimisho la kazi hii tuliyo kuwa tumekabidhiwa kuifanya.
Idara hii ni idara
ambayo inashuhulika na maswala
mbalimbali ya kitaaluma hapa chuoni (Elimu ya kimbingu na elimu ya
kidunia) kama ilivyo andikwa katika kitabu cha MITHALI 4:13, MKAMATE SANA ELIMU USIMWACHE AENDE ZAKE,MSHIKE MAANA
YEYE NI UZIMA WAKO’na lengo mahususi la idara
hii ni kuhakikisha wanachama wote wanakomaa katika elimu ya kimbingu na ya kidunia pia .
2:KAZI NA MALENGO YA IDARA
Idara ya elimu kwa mwaka wa kazi 2012/2013 ilikuwa
na malengo yafuatayo.
A.Kusaidiana na uongozi katika uratibu wa swala la
ruhusa za kimasomo kwa wanachama.
B.Kusimamia
mijadala ihusuyo program ya usomaji vitabu vya Roho ya unabii.
C:Kuibua na kukuza vipaji vya uhubiri ,uandishi na utoaji mihadhara kwa kushirikiana na idara ya programu na mambo ya kiroho.
D.Kusimamia uendashaji wa mafudisho mbalimbali ya
kiroho na kitaaluma kwa wanachama.
E. kusaidiana na uongozi wa kanisa ili kutoa msaada
wa kitaaluma kwa wanafunzi wa kiadvendista wanaosoma katika shule zinazo pakana karibu na chuo.
F: Kusimamia swala la ufunguzi wa library/maktaba ya
chama.
G.Kuanzisha jarida la chama.
MALENGO
YALIYO FANIKIWA:
A:Kusimamia
swala la ruhusa kwa wanachama pindi ratiba inapoingiliana na masaa ya Sabato.
Idara imekua ikitoa elimu kwa wanachama ili kutambua umuhimu wa kuiheshimu sabato,usajili
wa wanachama wote ili ufuatiliaji uwe rahisi,uteuzi wa wakilishi katika kila
course ilikurahisisha ufuatiliaji.
B:kukuza kiroho na kitaaluma wanafunzi wa sekondari
walioko jirani na chuo chetu.
·
Idara kwa kushirikiana na uongozi na
wanachama imefanikiwa kusaidia mwanafunzi
wa sekondari kitaaluma katika swala la
kumlipia ada na michango mingine binti
PENDO ZEBEDAYO kiasi cha shilingi-134,000/= kilitolewa kwa
mchanganuo ufuatao.-
ADA…………………………………………………(20000)
UKARABATI………………………………………(25000)
,RIM PAPER2……………………………………….(20000)
MICHANGO
MINGINE………………………… (69000).
=134000
. Aidha
uongozi unapenda kuwashukuru wanachama wote waliojitolea kumsaidia mwanafunzi huyu.
·
Idara imefanikiwa kutembelea shule
zilizoko jirani kwa ajili ya kutia moyo
wanafunzi .
Shule ya sekondari Sechelela ilitembelewa na mafundisho yaliyo fanyika ni
matatu(umuhimu wa kukamata elimu kama msingi wa maisha,kugawa vijiuzuu 140).
·
. Idara ilitembelea wana ASSA walio kuwa
katika mkutano mkuu wa conference kule capital Dodoma ili kuwahamasisha kupenda
neno la mungu lakini pia kujisomea sana hasa masomo ya sayansi ili kuongeza
wataalamu kwa siku zijazo.
·
Idara
kwa ushirikiano mzuri na wana kambi wa mahubiri ya ng’ong’ona
ilifanikiwa kutembelea shule ya sekondari ya ng’ong’ona .Ambapo tarehe
28/2/2012.kikosi cha watu 5 kilitumwa
hapo shuleni kuandaa mazingira ya kiwinjilisti. Mapokezi yalikuwa mazuri
sana tuliweza kuongea na wanafunzi wote.
·
Tarehe 2/3/2012. Kamati ilienda na
kikundi cha waimbaji na mzee wa kundi, vitabu 6 vya sabato ya kweli,vilitolewa
kwa wanachama wapya. Na vijizuu 8 vyenye masomo 15@ vilitolewa kwa wengine 8, faili
moja na madaftari 3 pamoja na kalamu 2 vilitolewa ili kuedesha shughuli za
wanafunzi hao. Na siku ya 3/3/2012 Wanachama
wapya 2 na wazamani 3 ambapo jumla ya shilingi 18500 wanafunzi zilitumika
katika hiyo kazi. Pesa hizo zilichangwa na wanakambi. Walibatizwa wawili na idara ilianza kuendesha
ibada hapo shuleni katika vipindi vya dini. Ambapo wastani wa watu 10-15 huwa
wanahudhulia mafundisho,vipindi hufanyika siku ya ijumaa saa 12;20-1;40pm.
·
Idara ilianzisha program ya elimu ya
watu wazima katika kundi la ng’ong’ona ili kusaidia wale washiriki wetu wasiojua
kusoma, ili wawe na uwezo wa kujisomea hata neno la Mungu. Huduma ilikuwa
ikitolewa ketika kundi la ng’ong’ona siku ya ijumaa saa 4;00pm -6;00pm, juma
pili saa 10;00am-12;00. Waalimu walikuwa ni wakujitolea.
C.KUSIMAMIA
MASOMO MBALIMBALI YANAYO ENDESHWA
CHUONI.
Kwa
kushirikiana na idara ya mambo ya kiroho masomo
mbalimbali yameendeshwa.
Masomo
yaliyoendwesha ni pamoja na
masomo ya juma la elimu kutoka conference yetu.
-
Masomo
mawili yenye kichwa kisemacho(NI WAKATI WA KUFIKIRI YALIYO JUU
Wakolosai 3:1-2) na somo
lingine ni ELIMU YA KIKRISTO NA UAMSHO NA
MATENGENEZO.
-Watu binafsi
wamekua wakiendelea kutoa masomo kama
yahusuyo utunzaji wa sabato,mwenendo wa mkristo. nk
D.KUHAMASISHA
WATU KUNUNUA VITABU ,KUSOMA NA KUGAWA.
-Idara inapenda
kushukuru wanachama ambao wameshiriki katika zoezi la ugawaji wa vitabu
(THE GREAT HOPE) kwa waalimu wetu takribani vitabu 600 vimetawanywa kwa wakufunzi wetu.
-vitabu vya( TUMAINI
KUU) vilivyo nunuliwa na wanachama
ni 853
sawa na shilingi 2,217,400/=
-Aidha idara inazidi kuwahimiza wanachama wazidi
kununua vitabu vya Roho ya unabii na kuvisoma ili kukua katika elimu ya
kiadvendista na kugawa kwa watu ambao
bado hawajajua elimu yetu/imani yetu.
E.KUIBUA
VIPAJI MBALIMBALI
Idara
inapenda kumshukuru MUNGU kwani
katika jambo hili kwa kushirikiana na
uongozi wa mambo ya kiroho vipaji mbalimbali
vimeibuliwa na kukuzwa. Mfano
tumefanya mikutano ya effort
za ndani na za nje ambazo wahubiri na waimbaji wametoka miongoni
mwetu .Hii ni njia mojawapo ya kukuza na
kuibua vipaji Mungu alivyo tujalia.
KUSIMAMIA SWALA LA UFUNGUZI WA MAKTABA YA CHAMA/LIBRARY.
Idara inapenda kumshukuru MUNGU, viongozi
wote na wanachama kwa
kufanikisha swala la ufunguzi wa maktaba
yetu. Ambayo ilizinduliwa rasmi
chuo cha mipango na mchungaji
Butoke katibu wa Conference yetu.
Vitabu
ambavyo vinapatikana katika maktaba yetu mpaka sasa ni vitabu 55.
Mchanganuo wake ni kama ifuatavyo.
THINK BIG VITABU 4@18600.............................................................................74400/=
STRESS AND ANXIETY 3@29500.........................................................................88500/=
FAMILY MEDICAL AID 3@19700.........................................................................59100/=
MUNGU KATIKA HISTORIA 3@3500..................................................................10500/=
JE MUNGU AWAJALI W AFRIKA 3@12800..........................................................38400/=
DHIKI KUU
3@7300....................................................................................................21900/=
UFUNUO WA MAMBO YAJAYO 5@13000..............................................................65000/=
HIGHLY EFFECTIVE MERRIAGE 2@53900............................................................53900/=
KUCHAGUA MCHUMBA 2@1600...........................................................................3200/=
SABATO YA KWELI 2@2500 ………………………………………………………5000/=
PATRIACHS AND PROPHETS 1@
7700……………………………………………7700/=
PROPHETS AND KINGS 1@7700…………………………………………………7700/=
KIFO NA UFUFUO 2@2000.....................................................................................4000/=
MAFUNDISHO YA BIBLIA
1@5500……………………………………………...5500/=
JIPATIE AMANI MOYONI
5@ 8000………………………………………………40000/=
SURVIVING FOR THE LOSS 1@28000……………………………………………28000/=
KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA 1 2 @16200 …………………………………32400/=
DANIELI NA SIKU ZETU 1@9500…………………………………………………9500/=
NUSURU NDOA YAKO
5@13000………………………………………………......65000/=
URITHI WA KANISA ………………………………………………………………….1O.
JUMLA=55.
VITABU 45 VILINUNULIWA NA
CHAMA KWA SHILINGI………………647,000/=
DAFTARI KUBWA 5 @2500……………………………...……………………12500/=
KWA UJUMLA
IDARA IMETUMIA SHILINGI 659,500/=
KATIKA SWALA LA MAKTABA YA CHAMA.
MATUMIZI MENGINE NI UNUNUZI WA FAILI,SH……………………………………………………………………….6000/=
KULIPA ADA YA MWANA FUNZI NTYKA SH
…………………....……. 134,000
KWA UJUMLA IDARA YA ELIMU MWAKA (2012-2013) IMETUMIA
KIASI CHA SHILINGI - 799500/=
SALIO KATIKA
IDARA….......................................………46500/=(KUTOKA KA TIKA
FEDHA ILIYOBAKIA KWA MWANAFUNZI NTYUKA.
CHANGAMOTO.
Pamoja na mafanikio ambayo kwa uweza wa Mungu pamoja na ushirikiano mzuri na uongozi mzima wa
chama umetupatia zipo changamoto ambazo bado zina ikabili idara hii kama ifuatavyo.
1.Bado baadhi ya
wanafunzi hawajawa na msimamo mzuri katika kusimamia swala la kutofanya mitihani siku ya Sabato hivyo wakati mwingine uongozi unapokua
ukifuatilia swala hili waalimu wetu
wanaona kama uongozi ndio unaoshinikiza watu kutofanya mitihani ila wao binafsi
wapo tayari.
2. Baadhi ya
wanachama wakati mwingine wanakua hawapo
tayari kushiriki katika huduma mbalimbali ili kukuza vipajia vyao .Mfano watu
wanapopangwa kuendesha program mbalimbali wanakataa,pia wakiambiwa wajitoe na kuendesha program mbalimbali
wanakuwa hawapo tayari.
3. Idara pia
haikufanikiwa kuanzisha jarida la chama ambalo
lilikua limekusudiwa kuandaliwa na idara kwa kushirikiana nawanachama
sababu ni kwamba maandalizi yake yalikua magumu ukizingatia mkakati wa kuanzisha ulikua unahusisha
kushirikisha kanisa lililokua lina tusimamia.
4. Wanachama wengi bado
hawajawa na muamko wakusoma vitabu
hasa Roho ya unabiiv hata vile
ambavyo viko kwenye maktaba bado wengine hawazimishi.
MAPENDEKEZO.
1.Idara inapenda
kupendekaza kwa uongozi ujao
kuendelea kutoa mafundisho yanayo husu swala la kuwa waaminifu kwa Mungu wetu hasa katika
kuheshimu masaa matakatifu ya sabato.
2.idara inashauri uongozi ujao uangalie nakufanya mchakato wa kuanzisha jarida la chama ambalo
litakua likitoa mafundisho yetu.
3.Idara inashauri
wanachama wote kufanya matengenezo katika swala la usomaji wa
maandiko matakatifu pamoja vitabu vyetu
vya Roho ya unabii ili kuweza kukua katika elimu ya kikristo.
4.Idara inapendekeza wanachama wote wajitoe katika kufanya program
mbalimbali kwani tunaamini kwamba
kila mtu anayo karama ambayo amepewa na Mungu na isipoitumia atadaiwa kwa hiyo kila mmoja ajue kwamba
sisi ni sawa na mwili mmoja na kila
kiungo ni muhimu ili kuweza kujenga mwili mzima.Kila mmoja awiwe kutoa kile alicho nacho kwa ajili
ya kujengana.
5.Idara inapenda
kutoaushauri kwa uongozi unaokuja kufanya namna ya kuengeza idadi ya vitabu vilivyoko katika maktaba yetu kwani mpaka sasa
vipo vitabu 55 tu ukilinganisha na idadi yetu wote wanachama ni vichache
sana.Hivyo tunapendekeza
ikiwezekana kufanyike changizo lingine ilituweze kupata fedha za
kuongeza idadi ya vitabu vyetu.
Pia mchungaji wetu mlezi
PASTOR Sulemani Mange alipendekeza
kwamba kule Marekani kuna vitabu vingi sana ambavyo tukifanya mipango kwa kumhusisha yeye twaweza kupata vitabu vingine
ili kukuza ukubwa wa maktaba yetu.
Hivyo tunapendekeza uongozi ujao ushirikiane na mchungaji wetu ili kufanikisha hili.
SHUKRANI.
Mwisho tunapenda kumshukuru MUNGU kwa uweza wake kutusimamia
katika kipindi chote cha uongozi mpaka hivi leo tuna kabidhi.
Tuna penda kushukuru
safu nzima ya uongozi chini ya
Mwenyekiti wetu Asubuhi Abayo kwa ushirikiano ambao tumeuonesha. Mungu awabariki sana.
Mwisho tunapenda kushukuru wanachama wote kwa ushirikiano
mkubwa mlio tupatia sisi viongozi wote
tulivuta pamoja ndio maana
tumefika hapa tulipo.Mungu
awabariki sana.
TAARIFA HII IMEANDALIWA NA
IDARA YA ELIMU-TUCASA UDOM
1 .SHAFII PETER MBWAMBO-----MKUU WA ELIMU
2. PAUL KIGWASHO
3. BONIFACE MWANGOMALE
4. BWANA MWITA
5. MOSABA MESHACK.
No comments:
Post a Comment