KANISA LA
WAADVENTISTA WASABATO
IDARA YA MAWASILIANO
CHUO
KIKUU CHA DODOMA
EMAIL: thisdasoudom@gmail.com
BLOGSPOT:
thisdasoudom.blogspot.com
TAAARIFA YA
UTENDAJI KAZI
DECEMBER 25, 2011 -
APRIL 4. 2013
VIONGOZI
1. ISAAC DOTTO MKUU (SOCIAL SCIENCE)
2. RAFAEL MWAMBENJA SOCIAL SCIENCE
3. ALLY KIBONA
HUMANITIES
4. MAPENZI JAMES
EDUCATION
5. KAZIMOTO TOBIAS
INFORMATICS
6. MTATILO EZEKIEL MEDICINE
YALIYOMO
1.
UTANGULIZI
2.
SHUKRANI
3.
MALENGO
4.
MAFANIKIO
5.
MAPATO NA MATUMIZI
6.
CHANGAMOTO
7.
MAONI
8.
MWISHO
UTANGULIZI
Idara ya
mawasiliano inapenda kuwaletea taarifa ya utendaji kazi tangu ilipokabiziwa
december 2011 hadi leo April 4, 2013.
1.
SHUKRANI
Tunapenda kumshukuru Mungu awali ya yote kwa uweza wake kwa kutuweka salama kuanzia
kipindi tulipoanza kazi hadi hivi leo. Pia tunapenda kuushukuru uongozi wa THISDASO-UDOM
chini ya mwenyeketi wake Abayo Asubuhi, Daniel Karangi pamoja na Gerald
Asubiswe, makatibu wote na idara zote za THISDASO chuo kikuu Dodoma. Hatuwezi
pia kuwasahau wanachama wenzetu kwa ushirikiano waliotupatia katika utendaji
kazi katika idara hii nyeti ya mawasiliano wote kwa pamoja tunawashukuru sana
na Mungu awabariki na kuwazidishia zaidi.
2.
MALENGO
Tangu kuanza kwa kipindi chetu cha
uongozi idara imekuwa na malengo mbalimbali katika makundi mawali, yaani
malengo ya muda mfupi nay ale ya muda mrefu.
2.1 MALENGO YA MUDA MFUPI
Haya ni malengo ambayo idara imekuwa
ikiyatendea kazi kwa ukaribu zaidi kuhakikisha idara inaendelea vizuri katika
utendaji wake. Malengo hayo ni kama ifuatavyo;
(i). idara ilidhamiria kuongeza vifaa
vya mawasiliano ambavyo vimekuwa vikitumika katika ibada zetu. Baadhi ya vifaa
idara ilivyodhamilia kuwa navyo ni kama ifuatavyo;
·
Hornspeaker 2 @tsh 150, 00
·
Keyboard organ PSR 7000 1,800,000
·
Wireless microphone 1 set
@ths 200,000
·
Flash 1, 4GB @ths 20,000
·
Modem 1 (multipurpose) @tsh 50,000
·
Microphone cover 10 @tsh 1000
·
Headphone 1 @ tsh 30,000
(ii). Idara ilidhamilia kuendelea
kutafuta chumba cha kuhifadhia vyombo vya mawasiliano
kutokana na changamoto zilizokuwepo mahali pa kuhifadhia vyombo.
(iii). Idara pia ilidhamiria kulihusisha
kanisa katika operation ya generator kwa kununua mafuta ya kila wiki ya ibada pindi panapotokea tatizo la
umeme.
(iv). Idara ilidhamiria kuendelea
kuiboresha blogspot ya chama kwa kuweka taarifa mbalimbali na masomo mbalimbali ambayo ingesaidia
kufikisha taarifa kwa wanachama katika
vitivyo vyetu.
(v). Idara ilidhamiria kubadilisha code za
usajili wa vyombo awali ikiwa ni T.UDOM/PA/CMPT/01
na kupendekezwa kuwa THISDASO/UDOM/PA/MIC/01.
(vi). Idara ilidhamiria kuvifanyia
mainteinance vyombo vya mawasiliano kila mara kuvilinda katika ubora wake kwa manufaa ya muda mrefu.
Tulitarajia kuwa na Tsh 1,000,000 kwa ajili
ya maintenance hii.
(vii). Idara illiahidi kuonyesha ushirikiano
kwa uongozi wote na idara mbalimbali katika utendaji
wa kazi ya Bwana. Aidha idara kwa kushirikiana na uongozi pamoja na wanachama ilikuwa ikitoa
vyombo maeneo nje na chuo chetu pindi vyombo vilipokuwa vikiombwa kwa shughuli mbalimbali.
(viii). Idara ilidhamiria kuwa na pesa ya
uchakavu TSH. 20,000 pindi vyombo vilipokuwa vikiombwa
kutumika nje na eneo letu.
(ix).
Idara ilidhamilia kujenga uhusiano mzuri kwa wanachama kwa kushirikiana
na wakuu wa program coordinators na wakuu
wa kiroho katika kendesha shughuli mbalimbali za kiroho chuoni kwetu.
(x). Idara ilidhamiria kuandaa DVD za matukio
mbalimbali za ibada zetu pamoja na mikutano mbalimbali
ya injili iliyokuwa ikifanyika katika uhusika wetu. Kwa mfano mikutano ya effort na uzinduzi
wa kwaya
zetu n.k.
(xi). Idara ilidhamiria kutohusika kuburn nyimbo au
album za kwayya mbalimbali zilizomo katika
maktaba yetu ya mawasiliano mbali idara ilidhamiria kutoa masomo na mafundisho yoyote pale
wanachama walipoyahitaji kwa kujifuanza zaidi.
(xii). Idara ilidhamiria kuendelea kushughulikia
tatizo la usafiri hasa siku za ibada licha ya changamoto mbalimbali
zinazojitokeza.
(xiii). Idara
ilidhamiria kuendelea kutoa taarifa za utendaji kazi wake katika kipindi hiki
cha uongozi hadi
mwisho wa uongozi pia.
MALENGO YA MUDA MREFU.
·
Idara ilidhamiria kuwa na harakati za
kuwa na gari la chama kwa ikiwa ni moja ya miradi ya chama. Hivyo kamati maalum
itaundwa kwa ajili ya kushughulikia suala hili ni vipi tutaweza kunua hili gari
pamoja na uedeshaji wake.
·
Idara ilidhamiria kununua photocopy
machine itakayo rahisisha upatikanaji wa nakala mbalimbali.
·
Idara pia ilidhamiria kuendelea kutoa
mafunzo mbalimbali ya utumiaji wa vifaa vya mawasiliano kwa wanachama wake.
·
Idara pia ilitarajia kuongeza vifaa
vingine vya mawasiliano kama vile video camera, external disk, stendi za
microphone na boxspeaker moja.
3.
MAFANIKIO
Tunamshukuru
Mungu katika malengo tuliyokuwa nayo katika kuyatekeleza katika kipindi hiki
cha uongozi. Idara imeweza kufanikiwa kutekeleza mambo yafuatayo;
1. Idara
imeweza kufanikiwa kuongeza baadhi ya vifaa kama vile cable 3 za microphone @
20,000, sponge 5 za microphone @2,000 na sanduku kwa alili ya kutunzia laptop
pamoja na projector kwa gharama ya Tsh 60,000.
2. Idara
pia imefanikiwa kuweza kupata chumba cha kuhifadhia vyombo vya mawasiliano
humanities kwa gharama ya Tsh 50,000 lakini upande wa COED bado tunachangamoto
ya chumba kwa ajili ya kuhifadhiwa vyombo vyetu vya mawasiliano ila tunaendelea
kufuatilia suala hilo.
3. Idara
imefanikiwa katika kulihusisha kanisa katika kulihudumia kundi la UDOM na
tumekuwa tukiendelea kupata mafuta kwa
ajili ya generator pale tulipokuwa na uhitaji huo.
4. Idara
imeendelea kushughulikia blogspot ya chama kwa kuweka taarifa mbalimbali
zinazohusiana na chama chetu ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali.
5. Idara
imefanikiwa kuonyesha ushirikiano na viongozi wengine katika idara tofauti
tofauti katika kufanya kazi mbalimbali katika idara husika.
6. Idara
imefanikiwa kuwa na pesa za uchakavu kiasi cha Tsh 20,000 pindi vyombo
vilipokuwa vikitumiaka nje ya eneo letu kama vile kwenye harusi na sehemu nyinginezo.
7. Idara
imefanikiwa kuwa na uhusiano mzuri na wanachama kwa kushirikiana na program
coordinators, na wakuu wa mambo ya kiroho katika kuendesha shughuli mbalimbali
za kiroho katika chuo chetu.
8. Idara
pia imefanikiwa kutengeneza DVD yenye matukio mbalimbali kama vile effort
zinazofanyika na mikutano ya ibada katika chuo chetu. DVD hizi zinapatikana
katika maktaba ya mawasiliano japo hazikutangazwa lasmi kuanza kuuzwa kwa
wanachama kwa gharama ya Tsh 1500.
9.
Idara imefanikiwa katika kujihusisha
kuburn DVD za nyimbo za album za kwaya au vikundi mbalimbali kwa ajili ya
kulinda kazi ya watu husika. Hivyo idara imekuwa ikitoa masomo na mafundisha
mbalimbali kwa njia ya softcopy kwa wale waliyoyahitaji masomo hayo.
10.
Idara inaendelea kushughulikia suala la
usafiri hasa siku za ibada japo changamoto bado ni nyingi katika suala hili la
usafiri.
11.
Idara imefanikiwa pia kufanya
maintanince ya vyombo vya mawasiliano ikiwemo na utengenezaji wa tyres za
generator.
KATIKA
MALENGO MAREFU
Idara kwa kushirikiana
na wakuu wengine wa idara imekuwa na kamati ikiwa chini ya mwenyekitii kwa
ajili ya kushughulikia miradi mbalimbali tunayoendelea kuifatilia ili ianze kufanya
kazi.
5. MAPATO NA MATUMIZI
5.1 MAPATO
Salio anzia…………………………………….220,900.00
Makusanyo……………………...……..315,500.00
Usafirishaji
P.A system……………….106,
500.00
Picha za
wahitimu 81@500……………..40,500.00
Pesa ya
uchakavu mkutano wa akina Mam…50,000.00
Pesa ya
uchakavu toka mahubiri ya zone(2013)..100,000.00
Pesa ya
uchakavu toka TU Retreat(2013)…50,000.00
Pesa ya
uchakavu toka Capital……………………………………………..20,000.00
Pesa ya
uchakavu katika harusi Dodoma kati...20,000.00
Jumla ya mapato………………………702,500.00
5.2 MATUMIZI YALIYOFANYIKA
Gharama za Usafirishaji wa P.A
System……45,000.00
Usafirishaji wan nje toka Dom kati.……..….25, 000.00
Matengenezo
ya vifaa (ndani)………….…..380,
400.00
Manunuzi
ya vitasa na
kufuli………………………………………………..8,000.00
Mawasiliano……...……………………..…2,500.00
Editing
passport size……………..…..……40,500.00
Ushafirishaji wa PA System………………..80,000.00
Matengenezo ya vifaa…………………..….70,000.00
Ununuzi
wa betri za microphone………..….2,500.00
Jumla ya Matumizi
yaliyofanyika…..….…653,900.00
Salio ishia la Idara ya Mawasiliano.......... 269,500.00
IDARA YA MAWASILIANO
Ongeza:
Makusanyo…………………………….….702,500.00
Jumla ya .……………………………..…923,400.00
Ondoa: Jumla ya Matumizi
yaliyofanyika…….…653,900.00
Salio ishia la idara ya
mawasiliano…………..…..269,500.00
6. CHANGAMOTO
Katika malengo yetu
hatukuweza kufanikisha malengo yote kuyatendea kazi kutokana na sababu
mbalimbali. kwa mfano hatukuweza kuongeza vifaa vyote kama ilivyo kwenye lengo
letu la kwanza kutokana na ufinyu wa pesa tulizokusanya katika changizo la PA
SYSTEM,
Pia hatujafanikiwa
kubadilisha codi ya PA SYSTEM Kama ilivyokuwa imependekezwa katika lengo letu
la tano kutokana na mafundi kutoeleweka.
Tatizo la usafiri bado
ni changamoto katika idara hii kutoka na wanafunzi wenzetu kutotoa pesa zao mapema
na kwa wakati hivyo tumekuwa tukilazimika wakati mwingine kutumia pesa zetu
mifukoni ili kuwezesha suala nzima la usafiri.
Kumekuwa na tatizo
kubwa la ubebaji wa vyombo vya mawasiliano hasa kwa wale wanaopangwa
kutoonekana hivyo kutupatia wakati mgumu na mzigo mkubwa wana idara katika
kuhakikisha vyombo vinafika mahali husika.
7.
USHAURI
Tunapenda kuwaomba
wanachama wenzetu kutupatia ushirikiano wa kutosha katika idara hii hasa katika
ubebaji. Idara hii si ya Mapenzi, mwambenja, kazimoto, Dotto, Kibona au
mtatilo. Tunahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wanachama wenzetu katika
kufanikisha idara hii. Tunawaomba sana.
Tunapenda pia kuwaomba
wanachama wenzetu kutoa pesa za nauli mapema ikiwezekana kuanzia juma tatu na
mwisho iwe ijumaa ili tujue idadi kamili ya watu na idadi ya magari
tutakayoleta. Siku ya sabato hatutapokea pesa ya mtu yoyote Yule.
8.
MAONI
Idara inapenda kuwasihi
viongozi wapya wa TUCASA wanaoanza kazi yao kutopokea pesa za uchakavu mikononi
mwao badala yake ziwekwe kwenye account na muhusika alete pay in slip kwa ajili
ya kuandikishana mkataba.
Viongozi wapya pia waendelee kufuatilia
projector kutoka kwa vice president wetu pr. Geofrey Mbwana aliyoahidi kipindi
cha retreat.
Tunapenda kuwaomba pia
viongozi wapya kusimamia vyombo pasipo kuwa na muungiliano wa mtu yoyote
asiyehusika katika idara hii ili kuondoa usumbufu katika kuoperate vyombo vya
mawasiliano. Hivyo mtu yoyote asiyehusika katika idara hii tuwaachie wanaidara
wenyewe wafanye kazi hiyo.
Tunawaomba pia
wanaidara wenzetu wanaoingia kuendelea kuiboresha blogspot yetu zaidi ya hata
pale tulipofanya sisi viongozi tunaomaliza mda wetu.
Pia tunawasihi wenzetu
kuongeza vyombo vya mawasiliano ikiwemo 1 set of wireless microphone kwa ajili
ya ufanisi wa ibada zetu.
9. MWISHO
Idara inawashukuru sana
wana TUCASA wote wa chuo kikuu cha Dodoma kwa namna tunavyoshirikiana katika
kuimaliza kazi ya bwana. MUNGU wetu wa
Mbinguni na atubariki sana. Zaidi tunapenda kuomba ushirikiano wenu hadi hapo
tutakapoimaliza kazi ya Bwana hapa duniani.
“LAKINI KATIKA MAMBO HAYO YOTE TUNASHIDA, NA ZAIDI YA KUSHINDA, KWA YEYE ALIYETUPENDA.”
WARUMI 8:37
Imeandaliwa na
IDARA YA MAWASILIANO
CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
2011/2013
No comments:
Post a Comment