Wanachama wa TUCASA waliohudhuria ziara hiyo ya mafunzo wakiwa na wenyeji wao
Tuesday, May 28, 2013
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Waadventista wa Sabato yaani TUCASA-UDOM hakika wamefurahi na kusema kuwa hakika hawatajuta kusoma katika chuo hicho ila pia hawatajuta kuwa na mlezi mzoefu katika mambo ya vijana PR. Suleiman Mange .
Maneno hayo yalisikika baada ya wanafunzi hao kutembelea eneo la uwekezaji la Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda lililopo Dodoma eneo la Zuzu na kujifunza mengi kuhusu ujasiliamali na wamesema kuwa hakika wamejifunza mengi sana na wamepata ni wapi pa Kuanzia
WanaTUCASA wakifurahia ufugaji wa mbuzi
Huko walitembelea maeneo na kujifunza masomo yahusuyo:
1. Ufugaji wa nyuki(somo lililowavutia wanaTUCASA wengi sana)
2. Ulimaji wa zabibu
3. Ulimaji wa nyanya,vitunguu na ndizi kisasa
4. Ufugaji wa mbuzi na kuku kisasa
5. Alizeti namna ya kulima na uvunaji wake kisasa
Hakika kuwa ndani ya Yesu kuna raha njoo ujifunze mengi kupitia TUCASA-UDOM unakaribishwa sana
Mungu awabariki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MUNGU awabaliki wote na awazidishie amani na upendo.
ReplyDelete