skip to main |
skip to sidebar
JE, WAJUA HISTORIA YA CHRISTMAS KWA UFUPI..??
Biblia haijaweka wazi tarehe aliyozaliwa YESU. Historia inaonyesha wazi
kuwa, tar 25/12 ni tarehe aliyozaliwa "Tammuz" ambaye wapagani
waliamini kuwa Tammuz ni mungu wa mimea na mazao, hivyo basi wapagani
waliazimisha kuzaliwa kwa Tammuz kila inapofika tarehe hiyo. Kanisa
chini ya kiongozi Constantine likaamua kuingiza siku hii kama siku ya
kuzaliwa YESU ili kuwavuta wapagani wajiunge na kanisa ili kuongeza
mapato ya kodi. SWALI.. Je kuna uhusiano gani kati ya kuzaliwa kwa YESU
na mti wa Christmas.??? Mti wa Christmas ni ishara ya kuzaliwa kwa
Tammuz ambaye wapagani waliamini kuwa ndiye mungu wa mimea na mazao.
HITIMISHO: Fanya Biblia pekee kuwa mwongozo wa maisha yako. KUMBUKA:
Biblia ndiyo katiba ya kikristo. Acha kufuata mapokeo.
Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. kama kuna fungu lolote linalosema Yesu alizaliwa tarehe 25/12 kwenye Biblia sema, na kama hakuna badilika kuanzia leo usiitukuze miungu ya babeli.
Mungu akubariki
No comments:
Post a Comment