Social Icons

Thursday, December 22, 2011

TAARIFA YA IDARA YA MAWASILIANO

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

nokia pictures 036

TANZANIA HIGHER LEARNING INSTITUTION SEVENTH DAY ADVENTIST STUDENT ORGANIZATION (THISDASO)

TAWI LA CHUO KIKUU CHA DODOMA

BLOGSPOT: http//: thisdasoudom.blogspot.com

EMAIL: thisdasoudom@gmail.com


IDARA YA MAWASILIANO

TAARIFA YA UTENDAJI KAZI

FROM JANUARY TO NOVEMBER 30, 2011

VIONGOZI

1. WANG’UBA, Joel S. (Mwenyekiti) 0767 120 787 / 0718 000 527

2. MABELE, Mtwale. (SSH) 0759 443 961 / 0713 775 295

3. SAMWEL, Murembe. (CIVE) 0764 490 744

4. MTATIRO, Ezekiel Geteyeye. (CHAS) 0765 479 868

5. EMANUEL, Elias. (CoED) 0756 058 582


YALIYOMO

Ø Shukurani

Ø Malengo

Ø Mafanikio

Ø Matarajio

Ø Mwisho


SHUKURANI

Tunapenda kumshukuru Mungu kwa uweza wake kwa kutuweka salama kuanzia mwanzo wa Masomo wa muhula wa mwaka uliopita na muhula huu pia. Pia tunapenda kuushukuru uongozi wa THISDASO – UDOM kwa kuwa Pamoja katika kipindi hiki chote cha uongozi tuliokabidhiwa na wenzetu walokuwa hapa kabla. Pia kwa wanachama wa THISDASO – UDOM ambao kwa namna moja au nyingine wamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya idara hii nyeti na muhimu katika utendaji kazi wa chama chetu pia kuhakikisha idara hii ikitenda kazi yake vyema na kutoa ushirikiano wa moja kwa moja pale walipohitajika kufanya hivyo, kwa mfano; ushauri wa kiufundi. Kutokana na shukurani hizo idara inaomba ushirikiano uliooneshwa kwetu uendelee kwa wengine watakaokabidhiwa idara hii.

MALENGO

Tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza cha utendaji kazi idara imekuwa na malengo mbalimbali ambayo kwa kifupi yamegawanyika katika makundi mawili (2), yaani; malengo ya muda mrefu na ya muda mfupi.

Malengo ya muda mfupi; haya ni malengo ambayo idara kutokana na ushauri kutoka kwa viongozi wengine wa tawi letu na wadau wa idara husika, idara iliona ni vyema kuyaweka katika malengo ya muda mfupi ambayo yatafanyiwa kazi kwa uharaka katika kipindi hiki cha uongozi kabla ya kukabidhi kwa wenzetu. Malengo haya yamekuja kwa sababu kuu za kiuinjilisti ambazo zilikuwa zinakwama kwa namna moja au nyingine.

Idara ilidhamiria kuongeza vifaa vya mawasiliano ambavyo vitatumika katika ibada za kawaida na mikutano ya hadhara ya kiuinjilisti. Vifaa vilivyotakiwa vimeorodheshwa hapa chini na bei zilizokuwa zimekadiriwa;

v Projector 1 1,000,000/=

v Generator 1 1,000,000/=

v Laptop 1 1,000,000/=

v Digital camera 1 250,000/=

v Horn speakers 4 600,000/=

v Modern 50,000/=

· Kuhamasisha wana- THISDASO - UDOM kutembelea blogspot ya chama. Hii ni njia mojawapo ya kupashana habari wakati tukiwa hapa chuoni na wakati wa likizo. Hivyo tuliona ni vyema tutoe ushauri kwa wanachama ili waweze kupata taarifa kwa wakati husika na kutoa taarifa popote wanapokuwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na uongozi.

· Kuvisajili (coding) vyombo vyote vya mawasiliano vya tawi letu la THISDASO - UDOM. Hii ni kwa ajili ya kutambua vyombo vyote vinavyomilikiwa na chama.

· Kuvifanyia matengenezo vyombo vyetu vya mawasiliano (maintenance).

Malengo ya muda mrefu;

· Kuongeza vifaa vya mawasiliano. Vifaa hivi ni Pamoja na

v Wireless microphones (1 set) 190,000/=

v Box speaker I 400,000/=

v Microphone stands 4@60,000/= 240,000/=

v Kinanda (Yamaha PSR 2100) 2,000,000/=

v Microphone cables 4@15,000/= 60,000/=

v Microphone head covers 8@ 1,000/= 8,000/=

v Ear phone 30,000/=


· Kuendesha mafunzo kwa wanachama (hasa wa mwaka wa kwanza) juu ya usimamizi wa vyombo vya mawasiliano na kuviendesha, kwa wanachama wanaowiwa kufanya hivyo kwa ajili ya kuacha ujuzi huo kwa wenzetu tunaowaacha.

· Kupata mahali rasmi pa kuhifadhia vyombo vya mawasiliano badala ya kuendelea kutunzwa katika vyumba vya wanachama kwa wakati tunapokuwa chuoni ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.

· Kuandaa siku maalum ya mawasiliano. Katika siku hiyo imepangwa pia kufanya changizo kwa ajili ya kuongeza vyombo vya mawasiliano. Pamoja na wanachama kuifahamu idara hiyo vyema na utendaji kazi wake ndani na nje ya tawi letu. Masomo mbalimbali ya kiroho yamepangwa kuendeshwa.

· Safari za wanachama wakati wa ibada na mikutano mikuu. Kwa kutambua kuwa idara inahusika moja kwa moja katika suala la kusimamia usafiri katika safari mbalimbali za wanachama ndani na nje ya chuo, idara imeazimia; kuhakikisha tarehe za mwisho za utoaji wa nauli za safari za mikutano mikuu ya chama (retreats) zinazingatiwa ili kuondoa usumbufu katika utafutaji wa usafiri ulio bora, wa kuwatosha na kuwafaa wanachama wanaosafiri. Pia usafiri wa ndani wa kutoka kitivo kimoja kwenda kingine kwa ajili ya ibada. Idara imeona ni vyema kwa wanachama kutoa pesa kwa wakati ili kupunguza usumbufu wa usafiri kwa siku ya sabato. Kuhakikisha usafiri unapatikana kwa wanachama wote walio katika mpango maalum tunapotoka nje ya chuo kwa ajili ya ibada za kanda.

MAFANIKIO

Idara ya mawasiliano katika kipindi chake cha utendaji kazi imefanikiwa katika kukamilisha mambo yafuatayo ambayo ilijipangia kuyafanya wakati wa uongozi wao;

· Kuwa na siku ya mawasiliano ambapo kwa pamoja tulipata wasaa wa kujifunza neno la Mungu katika ibada ya sabato hiyo iliyofanyika BREAK POINT CAFTERIA. Pamoja na hilo, siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kufanya changizo kwa ajili ya kufanya ununuzi wa vifaa vya mawasiliano vilivyokuwa vinapungua kama ilivyoelezwa hapo kabla. Katika kuhakikisha siku hiyo inafanikiwa, kamati maalum iliundwa ili kusimamia na kuhakikisha malengo katika siku hiyo yanafanikiwa na kufanyika kwa usahihi.


Kamati hiyo iliundwa na watu wafuatao;


MABELE, Mtwale. Mwenyekiti

MORISS, Frank. Katibu

MWILIMA, Emmanuel Mjumbe

NYANDO, Adam Mjumbe

LAMECK, Hezron Mjumbe

· Kuongeza vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya kurahisisha kazi ya uinjilisti na kuboresha vipindi mbalimbali vya ibada. Vifaa vilivyoongezwa ni pamoja na;

§ Projector 1 1,007,000/=

§ Generator 1 1,350,000/=

§ Laptop 1 682,000/=

§ Digital camera 1 240,000/=

§ Laptop bag 30,000/=

§ Extension cable 8,000/=

§ Memory card ya camera 25,000/=

Taarifa ya manunuzi ya vifaa hivi inaambatana na taarifa hii ya utendaji kazi


· Kwa safari za kutoka nje ya tawi, idara imefanikiwa kuendelea kutekeleza majukumu iliyojipangia ingawaje kumekuwa na changamoto za hapa na pale. Hii inasababishwa na baadhi ya wanachama ambao wamekuwa hawatoi fedha za nauli kwa muda na wakati husika hivyo kufanya zoezi kuwa gumu. Kwa wale ambao hutoa wengine hutoa kiasi pungufu hivyo kuuachia uongozi mzigo mzito hasa katika kuingia katika makubaliano na vyombo vya usafirishaji (mabasi) ya abiria.

· Kuvisajili vyombo vyote vya mawasiliano. Idara ilisajili vyombo vyote kwa kuvipa alama ya T.UDOM/PA/……/……

· Kufanya mafunzo kwa mwanachama mmoja kuhusu kuvifunga na kuvilinda vyombo visiharibike. Hivyo uongozi unaoondoka bado utatoa nafasi kwa wengine kuja kujifunza ili waweze kuvifunga kwa usahihi zaidi na kwa utaalamu.

CHANGAMOTO (malengo ambayo hayakutimia)

· Kuongeza kwa vifaa vya mawasiliano kama vile spika, microphone stand na spika(horn speaker). Hii imetokana na mfuko wa idara kutokuwa na pesa ya kutosha kwa ajili ya manunuzi ya vifaa hivyo. Lakini pia, michango mingine iliyochangwa kwa ajili ya vifaa vya mawasiliano bado haijafika tawini kutokea kanisani

· Ununuzi wa moderm kwa ajili ya shughuli za kichama .

· Utoaji/uchangiaji wa pesa za nauli kwa wakati. Hili limefanya viongozi wa mawasiliano kuwa katika wakati mgumu baada ya kufanya makubaliano na wenye magari. Hivyo idara imekuwa na changamoto kubwa katika zoezi hili.

· marekebisho (maintenance& repair) kwa vyombo vyetu vya mawasiliano. Hii imetokana na kuwa na mambo mengi ya kufanya katika wakati wa uongozi.

· Wanachama kutotembelea blogspot ya chama. Hivyo hili limeleta changamoto kubwa kwa utendaji kazi mana kuna wakati matangazo muhimu katikati ya wiki yanawekwa katika blog lakini wengi wa wanachama hawaonekani kuwa na taarifa hizo. Hivyo kwa uchunguzi uliofanyika wanachama wengi hawatembelei blogspot ya chama.

Bajeti ya idara ilikuwa ni Tshs. 5,000,000/= iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya matumizi ya idara.

VYOMBO VYA MAWASILIANO VILIVYOPO MPAKA SASA.

Mpaka sasa idara ya mawasiliano kwa niaba ya THISDASO – UDOM ina idadi ya vifaa vyenye thamani ya Tshs. 5,934,500/=. Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:

v Box Spika 2

v Stand 2 za spika

v Stand 1 ya microphone

v Mixer 1

v Mic : wireless 1 set

v Cable 6

v Printer 1

v Projector 1

v Laptop 1

v Bag la laptop 1

v Memory card ya camera 1

v Generator 1

v Digital camera 1

v Antivirus 1

v Stabilizer 1

v Extension cable 3

v Speaker`s cable

USHAURI:

Idara ya mawasiliano inayomaliza muda wake inapenda kutoa ushauri ufuatao:

· Wanachama kuwa waaminifu kwa yale mambo ambayo tunakubaliana kama vile kutoa pesa za nauli kwa wakati ili kuondoa usumbufu.

· Kufanya upya usajili wa vyombo vyote vya THISDASO UDOM kwa kuweka alama itakayokubaliwa na wanachama na uongozi kwa ujumla wao. Hivyo idara ihakikishe zoezi hili linafanyika kwa wakati.

· Kuvitumia vyombo vyetu vizuri ili kwamba viweze kutusaidia sisi na ndugu zetu watakaokuja nyuma yetu. Hivyo kwa kila atakayepewa kazi ya kuvifunga(kuviandaa) anatakiwa kuwa makini kwa kile atakachokuwa anafanya kwa ajili ya kulinda vyombo vyetu visiharibike.

· Kuviimarisha/kuboresha vyombo vyetu vya mawasiliano kwa kuvipeleka kwa fundi kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho madogo madogo (maintenance & repair) ili viweze kufanya kazi yake ipasavyo. Hivyo idara inatakiwa kulichukua jambo hili kwa uzito zaidi na umuhimu wake.

· Kutafuta sehemu ya kuhifadhia vyombo vyetu. Uongozi unaoondoka madarakani umejitahidi kwa kila ilivyowezekana Kupata mahali pa kuhifadhia vyombo vyetu. Hivyo basi mpaka tunamaliza muda wa uongozi, uongozi wa chuo haujatupatia jibu rasmi la kupewa au kutopewa sehemu ya kuhifadhia vyombo hivyo. Hivyo uongozi unaoondoka unaomba uongozi mpya ulifuatilie jambo hili kwa ukaribu zaidi.

Kuweka malengo ya kununua gari kwa ajili ya matumizi ya chama na kupunguza adha ya usafili kwa wanachama siku ya SABATO

MWISHO

Uongozi unaoondoka madarakani unapenda kuwatia moyo wale ambao wamekabidhiwa idara hii. Hivyo viongozi wanaoachia madaraka wako tayari kwa ajili ya kutoa ushauri na maelekezo mbalimbali kwa ajili ya utendaji kazi wa idara hii. Uongozi unaoingia madarakani unayo fursa ya kupewa ushauri wa kiufundi na wa kimawazo kutoka kwa wenzao.

Mungu atubariki sote na aendelee kutupa nguvu ya kuendelea kuifanya kazi yake tukisimama thabiti kama ndugu wa familia moja shambani mwake kwa ajili ya kumaliza kazi yake.

MUNGU NA AWABARIKI NYOTE

MATHAYO 28: 19 - 20

Taarifa hii imeandaliwa na idara ya mawasiliano na kupitishwa na mwenyekiti wa tawi la THISDASO – UDOM 2011.

WEBIRO, Ryakitimbo. A

DATE: …………………………….

SIGNATURE:…………………………

No comments:

Post a Comment