Social Icons

Featured Posts

Sunday, August 3, 2014

Wapendwa Makambi yamefika!

Msimu wa Makambi umefika wapendwa, Tufanye hima kuhudhuria mikutano hii muhimu kokote tulipo. Pia, tukumbuke kuwaalika ndugu jamaa na marafiki ili wote tupate baraka Hizi. Mungu awabariki!

Zaburi 32:1-2
1. Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.
2. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila.

Wednesday, May 7, 2014

PICHA ZA MAHAFALI 2014 -TUCASA DODOMA ZONE

Zifuatazo ni picha za mahafali mwaka 2014 TUCASA-DODOMA ZONE yaliyofanyika UDOM katika Cafeteria ya break point.
Tazama picha ni jinsi gani mahafali hayo yalipendeza

Huu ni wakati wa marching wahitimu kuingia ukumbini




Endelea hapo kupata nyingine ziko nyingi tu

Tuesday, April 29, 2014

JAMBO MUHIMU SABATO IJAYO

Tunapenda kuwakumbusha wanachama wote wa TUCAS-UDOM kuwa sabato ijayo 3/5/2014 tutasali College of Education, Tutakuwa na  meza ya Bwana katika sabato hiyo, hvyo tuandae mioyo yetu kushiriki huduma hiyo takatifu.
Mungu awabariki mnapojiandaa.

Monday, April 28, 2014

MAHAFALI YAMEFIKA

Wapendwa tunawakumbusha kuwa mahafali ya TUCASA kanda ya Dodoma yamefika kwani ni tarehe 4/5/2014 kumbuka kuwa tunapaswa kushirikiana na wenzetu kwa kuwaaga na kuwatakia baraka za Bwana,







 Hivyo kama hujatoa mchango wako kumbuka kutoa kwa mhazini wako wa tawi na mwisho wa kutoa ni tarehe 30/4/2014. jitahidi tushirikiane pamoja katika mambo yote.Mungu awabariki.