Social Icons

Saturday, May 4, 2013

TAARIFA YA IDARA YA ELIMU 2011/2013



            IDARA YA ELIMU-TUCASA UDOM

TAARIFA YA UTENDAJI KAZI  MWAKA 2O12/2013.
Taarifa hii ya    utendaji   kazi  wa idara ya elimu   TUCASA UDOM kwa mwaka wa uongozi 2012/2013 imegawanyika katika  sehemu    kuu nane( 8) ambazo ni.
1.Utangulizi.
2.kazi na malengo  ya  idara.
3.Malengo yaliyofanikiwa.
5. Fedha, bajeti na  matumizi.
6.Changamoto.
7.Maoni na mapendekezo.
8.Hitimisho.
                                    1.UTANGULIZI:
 Kwanza kabisa tunapenda kumshukuru MUNGU  kwa uweza wake  wa kutulinda tangu tumeanza uongozi mpaka leo tunapofikia hitimisho la kazi hii tuliyo kuwa tumekabidhiwa kuifanya.
Idara hii ni idara  ambayo inashuhulika na maswala  mbalimbali ya kitaaluma hapa chuoni (Elimu ya kimbingu na elimu ya kidunia) kama ilivyo andikwa katika kitabu cha MITHALI  4:13, MKAMATE  SANA ELIMU USIMWACHE AENDE ZAKE,MSHIKE MAANA YEYE NI UZIMA WAKO’na lengo mahususi la idara   hii ni kuhakikisha wanachama wote wanakomaa katika  elimu ya kimbingu na ya kidunia pia .

 
                                       2:KAZI  NA MALENGO YA IDARA
Idara ya elimu kwa mwaka wa kazi 2012/2013 ilikuwa na malengo  yafuatayo.
A.Kusaidiana na uongozi katika uratibu wa swala la ruhusa za kimasomo kwa wanachama.
B.Kusimamia  mijadala  ihusuyo  program ya usomaji vitabu vya Roho ya unabii.
C:Kuibua na kukuza vipaji  vya uhubiri ,uandishi na utoaji mihadhara  kwa kushirikiana na idara  ya programu na mambo ya kiroho.
D.Kusimamia uendashaji wa mafudisho mbalimbali ya kiroho  na kitaaluma kwa wanachama.
E. kusaidiana na uongozi wa kanisa ili kutoa  msaada  wa kitaaluma  kwa wanafunzi  wa kiadvendista wanaosoma  katika shule zinazo pakana karibu na chuo.
F: Kusimamia swala la ufunguzi wa library/maktaba ya chama.
G.Kuanzisha  jarida la chama.

MALENGO YALIYO FANIKIWA:
A:Kusimamia swala la ruhusa kwa wanachama pindi ratiba inapoingiliana na masaa ya Sabato.
Idara imekua ikitoa elimu kwa wanachama ili  kutambua umuhimu wa kuiheshimu sabato,usajili wa wanachama wote ili ufuatiliaji uwe rahisi,uteuzi wa wakilishi katika kila course ilikurahisisha ufuatiliaji.
B:kukuza  kiroho na kitaaluma wanafunzi wa sekondari walioko jirani na chuo chetu.
·         Idara kwa kushirikiana na uongozi na wanachama imefanikiwa  kusaidia  mwanafunzi  wa sekondari kitaaluma katika swala la   kumlipia ada na michango mingine binti   PENDO   ZEBEDAYO  kiasi cha shilingi-134,000/= kilitolewa kwa mchanganuo ufuatao.-
ADA…………………………………………………(20000)
UKARABATI………………………………………(25000)
,RIM PAPER2……………………………………….(20000)
 MICHANGO  MINGINE………………………… (69000).
                                                                                    =134000
.  Aidha uongozi unapenda  kuwashukuru  wanachama wote waliojitolea  kumsaidia mwanafunzi             huyu.
·         Idara imefanikiwa kutembelea shule zilizoko jirani  kwa ajili ya kutia moyo wanafunzi .
Shule ya sekondari  Sechelela ilitembelewa  na mafundisho yaliyo fanyika ni matatu(umuhimu wa kukamata elimu kama msingi wa maisha,kugawa vijiuzuu 140).
·         . Idara ilitembelea wana ASSA walio kuwa katika mkutano mkuu wa conference kule capital Dodoma ili kuwahamasisha kupenda neno la mungu lakini pia kujisomea sana hasa masomo ya sayansi ili kuongeza wataalamu kwa siku zijazo.
·         Idara  kwa ushirikiano mzuri na wana kambi wa mahubiri ya ng’ong’ona ilifanikiwa kutembelea shule ya sekondari ya ng’ong’ona .Ambapo tarehe 28/2/2012.kikosi cha watu 5 kilitumwa  hapo shuleni kuandaa mazingira ya kiwinjilisti. Mapokezi yalikuwa mazuri sana tuliweza kuongea na wanafunzi wote.
·         Tarehe 2/3/2012. Kamati ilienda na kikundi cha waimbaji na mzee wa kundi, vitabu 6 vya sabato ya kweli,vilitolewa kwa wanachama wapya. Na vijizuu 8 vyenye masomo 15@ vilitolewa kwa wengine 8, faili moja na madaftari 3 pamoja na kalamu 2 vilitolewa ili kuedesha shughuli za wanafunzi hao. Na siku ya 3/3/2012 Wanachama  wapya 2 na wazamani 3 ambapo jumla ya shilingi 18500 wanafunzi zilitumika katika hiyo kazi. Pesa hizo zilichangwa na wanakambi.  Walibatizwa wawili na idara ilianza kuendesha ibada hapo shuleni katika vipindi vya dini. Ambapo wastani wa watu 10-15 huwa wanahudhulia mafundisho,vipindi hufanyika siku ya ijumaa saa 12;20-1;40pm.
·         Idara ilianzisha program ya elimu ya watu wazima katika kundi la ng’ong’ona ili kusaidia wale washiriki wetu wasiojua kusoma, ili wawe na uwezo wa kujisomea hata neno la Mungu. Huduma ilikuwa ikitolewa ketika kundi la ng’ong’ona siku ya ijumaa saa 4;00pm -6;00pm, juma pili saa 10;00am-12;00. Waalimu walikuwa ni wakujitolea.
C.KUSIMAMIA MASOMO MBALIMBALI   YANAYO ENDESHWA CHUONI.
Kwa  kushirikiana na idara ya mambo ya kiroho  masomo  mbalimbali yameendeshwa.
Masomo  yaliyoendwesha ni pamoja na  masomo ya juma la elimu kutoka conference yetu.
-          Masomo  mawili  yenye  kichwa kisemacho(NI WAKATI WA KUFIKIRI YALIYO JUU  Wakolosai 3:1-2)  na somo lingine ni   ELIMU YA KIKRISTO NA UAMSHO NA  MATENGENEZO.
-Watu binafsi wamekua  wakiendelea kutoa masomo kama yahusuyo utunzaji wa sabato,mwenendo wa mkristo. nk
D.KUHAMASISHA WATU KUNUNUA VITABU ,KUSOMA NA KUGAWA.
-Idara inapenda  kushukuru wanachama ambao wameshiriki katika zoezi la ugawaji wa vitabu (THE GREAT HOPE)  kwa waalimu wetu  takribani vitabu 600 vimetawanywa kwa  wakufunzi wetu.
-vitabu vya( TUMAINI KUU) vilivyo nunuliwa  na wanachama ni  853  sawa na shilingi 2,217,400/=
-Aidha idara inazidi kuwahimiza wanachama wazidi kununua vitabu vya Roho ya unabii na kuvisoma ili kukua katika elimu ya kiadvendista na kugawa kwa watu  ambao bado  hawajajua elimu yetu/imani yetu.
E.KUIBUA VIPAJI MBALIMBALI
Idara  inapenda kumshukuru MUNGU  kwani katika jambo hili  kwa kushirikiana na uongozi wa mambo ya kiroho vipaji mbalimbali  vimeibuliwa na kukuzwa. Mfano  tumefanya mikutano ya  effort za  ndani na za nje  ambazo wahubiri na waimbaji wametoka miongoni mwetu .Hii ni njia mojawapo ya  kukuza na kuibua vipaji Mungu alivyo tujalia.
 KUSIMAMIA SWALA LA UFUNGUZI WA  MAKTABA YA CHAMA/LIBRARY.
Idara inapenda kumshukuru MUNGU,  viongozi  wote na wanachama   kwa kufanikisha swala la ufunguzi wa maktaba  yetu. Ambayo  ilizinduliwa rasmi chuo cha mipango na mchungaji   Butoke  katibu wa  Conference yetu.
 Vitabu ambavyo vinapatikana katika maktaba yetu mpaka sasa ni vitabu  55.
Mchanganuo wake ni kama ifuatavyo.

THINK BIG VITABU  4@18600.............................................................................74400/=
STRESS AND ANXIETY 3@29500.........................................................................88500/=
FAMILY MEDICAL AID 3@19700.........................................................................59100/=
MUNGU KATIKA HISTORIA 3@3500..................................................................10500/=
JE MUNGU AWAJALI W AFRIKA 3@12800..........................................................38400/=
DHIKI KUU 3@7300....................................................................................................21900/=
UFUNUO WA MAMBO YAJAYO 5@13000..............................................................65000/=
HIGHLY EFFECTIVE MERRIAGE 2@53900............................................................53900/=
 KUCHAGUA  MCHUMBA 2@1600...........................................................................3200/=
SABATO YA KWELI 2@2500 ………………………………………………………5000/=
PATRIACHS AND PROPHETS 1@ 7700……………………………………………7700/=
PROPHETS AND KINGS 1@7700…………………………………………………7700/=
KIFO NA UFUFUO 2@2000.....................................................................................4000/=
MAFUNDISHO YA BIBLIA 1@5500……………………………………………...5500/=
JIPATIE AMANI MOYONI  5@ 8000………………………………………………40000/=
SURVIVING FOR THE LOSS 1@28000……………………………………………28000/=
KUTAYARISHA NJIA SEHEMU YA 1  2 @16200 …………………………………32400/=
DANIELI NA SIKU ZETU 1@9500…………………………………………………9500/=
NUSURU NDOA YAKO  5@13000………………………………………………......65000/=
URITHI WA KANISA ………………………………………………………………….1O.

JUMLA=55.
VITABU 45 VILINUNULIWA  NA  CHAMA KWA SHILINGI………………647,000/=
DAFTARI KUBWA 5 @2500……………………………...……………………12500/=
 KWA UJUMLA IDARA IMETUMIA SHILINGI   659,500/= KATIKA   SWALA LA  MAKTABA YA CHAMA.

MATUMIZI MENGINE NI UNUNUZI  WA FAILI,SH……………………………………………………………………….6000/=
KULIPA ADA YA MWANA FUNZI  NTYKA SH   …………………....……. 134,000
KWA UJUMLA IDARA YA ELIMU MWAKA (2012-2013) IMETUMIA KIASI CHA SHILINGI -  799500/=
SALIO    KATIKA IDARA….......................................………46500/=(KUTOKA KA TIKA  FEDHA  ILIYOBAKIA  KWA MWANAFUNZI NTYUKA.      
CHANGAMOTO.
Pamoja na mafanikio ambayo  kwa uweza wa Mungu pamoja  na ushirikiano mzuri na uongozi mzima wa chama  umetupatia zipo changamoto ambazo  bado zina ikabili idara hii kama ifuatavyo.
                              
1.Bado baadhi  ya  wanafunzi hawajawa na msimamo mzuri katika  kusimamia swala  la kutofanya mitihani siku ya Sabato  hivyo wakati mwingine uongozi unapokua ukifuatilia swala hili  waalimu wetu wanaona kama uongozi ndio unaoshinikiza watu kutofanya mitihani ila wao binafsi wapo tayari.

2. Baadhi ya wanachama  wakati mwingine wanakua hawapo tayari kushiriki katika huduma mbalimbali ili kukuza vipajia vyao .Mfano watu wanapopangwa  kuendesha  program mbalimbali  wanakataa,pia wakiambiwa  wajitoe na kuendesha program mbalimbali wanakuwa hawapo tayari.
3. Idara pia haikufanikiwa kuanzisha jarida la chama ambalo  lilikua limekusudiwa kuandaliwa na idara kwa kushirikiana nawanachama sababu ni kwamba maandalizi yake yalikua magumu ukizingatia  mkakati wa kuanzisha ulikua unahusisha kushirikisha kanisa lililokua lina tusimamia.
4. Wanachama wengi bado hawajawa na muamko wakusoma vitabu  hasa  Roho ya unabiiv hata vile ambavyo  viko kwenye  maktaba bado wengine hawazimishi. 
MAPENDEKEZO.
1.Idara inapenda  kupendekaza kwa uongozi ujao  kuendelea  kutoa mafundisho  yanayo husu swala la   kuwa waaminifu kwa Mungu wetu hasa katika kuheshimu  masaa matakatifu   ya sabato.  
2.idara inashauri uongozi ujao  uangalie nakufanya mchakato  wa kuanzisha jarida la chama ambalo litakua  likitoa mafundisho yetu.
3.Idara inashauri  wanachama wote kufanya matengenezo katika swala la usomaji  wa   maandiko matakatifu pamoja vitabu vyetu  vya Roho ya unabii ili kuweza kukua katika elimu ya kikristo.
4.Idara inapendekeza wanachama wote  wajitoe katika kufanya program mbalimbali  kwani tunaamini  kwamba  kila mtu anayo karama ambayo amepewa na Mungu na isipoitumia  atadaiwa kwa hiyo kila mmoja ajue kwamba sisi  ni sawa na mwili mmoja na kila kiungo ni muhimu  ili kuweza  kujenga mwili mzima.Kila mmoja awiwe   kutoa kile alicho nacho kwa  ajili  ya kujengana.
5.Idara inapenda  kutoaushauri kwa uongozi unaokuja kufanya  namna ya kuengeza  idadi ya vitabu vilivyoko katika  maktaba yetu kwani  mpaka sasa   vipo vitabu 55 tu ukilinganisha na idadi yetu wote wanachama ni vichache sana.Hivyo tunapendekeza  ikiwezekana  kufanyike  changizo lingine ilituweze kupata fedha za kuongeza  idadi ya vitabu vyetu.
Pia  mchungaji   wetu mlezi    PASTOR Sulemani  Mange alipendekeza kwamba kule Marekani kuna vitabu vingi sana ambavyo tukifanya mipango kwa  kumhusisha yeye twaweza kupata vitabu vingine ili kukuza   ukubwa wa  maktaba yetu.  Hivyo tunapendekeza uongozi ujao ushirikiane na   mchungaji wetu ili kufanikisha hili.

SHUKRANI.
Mwisho tunapenda kumshukuru MUNGU kwa uweza wake kutusimamia   katika kipindi chote cha uongozi  mpaka hivi leo  tuna kabidhi.
Tuna penda  kushukuru safu nzima ya uongozi chini ya  Mwenyekiti wetu   Asubuhi  Abayo kwa ushirikiano ambao tumeuonesha.  Mungu awabariki sana.
Mwisho tunapenda kushukuru wanachama wote kwa ushirikiano mkubwa  mlio tupatia sisi viongozi  wote  tulivuta pamoja ndio maana  tumefika  hapa tulipo.Mungu awabariki sana.

TAARIFA HII   IMEANDALIWA   NA IDARA YA ELIMU-TUCASA   UDOM
1 .SHAFII   PETER MBWAMBO-----MKUU WA ELIMU
2. PAUL   KIGWASHO
3. BONIFACE   MWANGOMALE
4. BWANA   MWITA
5. MOSABA MESHACK.

No comments:

Post a Comment