Social Icons

Monday, April 28, 2014

PICHA ZA VIONGOZI WANAOENDA KUKABIDHI

 Hawa ni viongozi wa TUCASA_UDOM 2013/2014 wanaojiandaa kukabidhi jmosi ijayo tarehe 3/5/2014. Wakiwa katika picha  za pamoja katika kikao chao cha mwisho kilichofanyika college of Informatics and Virtual Education(CIVE) wakiwa pamoja na Pastor Baraka Butoke

Viongozi katika picha ya pamoja



Viongozi katika picha ya pamoja



Mwenyekiti anaemaliza muda wake Lazaro Moris(kushoto) akiwa na mwenyekiti anaeingia Sunday Aron(kulia) 

Monday, March 31, 2014

UZINDUZI WA VOL 4 Audio Cd YA SINAI-UDOM SDA CHOIR

Hizi ni picha za tukio hilo la uzinduzi lililofanyika katika kanisa la waadventista wa Sabato Kizota hapa Dodoma




PICHA ZA SEMINA YA ELIMU

Hizi ni picha mbalimbali za siku ya semina ya Elimu iliyofanyika College of Informatics and Virtual Education(CIVE-UDOM) zilizoendeshwa na Madam Devotha kutoka Eastern Tanzania Coference akiwa kiongozi wa Elimu.
Pastor Baraka Butoke akija na Seven word testemony                     

 The Heirs wakiimba




Watu wakiwa makini kutazama na Kusikiliza kinachoendelea. ilikuwa ni siku ya pekee sana
 Madam Devotha akija na somo linalosema "Kutazama sana"
UDOM  SDA Choir wakiimba

Tuesday, March 25, 2014

SEMINA YA ELIMU

Tunapenda kuwatangazia kuwa tarehe 28/04/2014 kutakuwa na semina kubwa ya Elimu(How to score high) itakayoendeshwa na Kiongozi wa idara ya Elimu toka ETC katika College of Informatics and Virtual Education Venue ni FL1 kuanzia saa 1:30 jioni  hadi saa 4 usiku. Jitahidi uje upate elimu itakayosaidia maisha yako kwaya mbali mbali zitahudumu kama vile Edeni-Udom,Sinai-Udom, Calvary-Udom,Haleluya-Udom na Tumaini-Udom.
Mungu awabariki mnapopanga kuhudhuria

SABATO MAALUM

Tunapenda kuwatangazia kuwa katikati ya Effort tunazoendelea nazo tumepata mbaraka wa  pekee. Pamoja na kuwa na semina ya elimu itakayofanyika College of Informatics and Virtual Education tarehe 28/03/2014 siku ya ijumaa kuanzia saa 1:30 jioni hadi 4:00 usiku Lakini pia siku ya jumamosi tarehe 29/03/2014 tutasali na wahadhiri wetu katika school of Humanities kuanzia asubuhi hadi jioni wakitufundisha mambo mbali mbali yanayohusu maisha kwa ujumla. Fika bila kukosa, njoo na rafiki yako tujifunze pamoja.
Mungu akubariki unajiandaa na sabato hiyo

Sunday, March 23, 2014

RETREAT STUM

Tunapenda kuwakumbusha wanaTUCASA wote kuwa Retreat yetu ya SOUTHERN TANZANIA UNION MISSION(STUM) imekaribia sana na kumbuka mwisho wa viingilio ni tarehe 30/3/2014 kwa hiyo tujitahidi sana wapendwa tukamilishe.
Mungu awabariki sana.